Watu
wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena
ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha
kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko
unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni
mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema
hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua.
Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.
Tamthilia
za Kiingereza na Kihindi zinazoonyeshwa hapa Tanzania watu wengi
huzielewa ilhali hawajui Kiingereza wala Kihindi. Kwa nini? Kwa sababu
wako makini na matendo ya wahusika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...

Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.
ReplyDeleteNukuu hii inahusu zile tabia za ndani kabisa ambazo aghalabu watu huwa hawataki kuzionyesha kwa sababu za kinafiki. Si kila tabia. Tabia zingine ni za kuzidharau. Mtu akikuonyesha tabia yake ya ndani kabisa itakayoweza hata kukushtua wewe, tabia ambayo hajawahi kuionyesha hata mara moja, kuwa makini naye. Kwa sababu anayajua maisha yake kuliko wewe unavyoyajua.
ReplyDeleteMtu hajawahi kuwa mwizi lakini leo kaiba, na umejua kwamba kaiba, amini kwamba ni mwizi.
ReplyDelete