Thursday, 24 November 2016

Mpelelezi wa Tume ya Dunia Frederik Mogens

Hellerup, Copenhagen, Denmaki, kitongoji cha matajiri wa Copenhagen katika pwani ya ukanda wa bahari wenye hadhi ya kimataifa ya Bendera ya Bluu wa Øresund (Sound, Sauti) ukanda wa bahari unaotenganisha kisiwa cha Denmaki cha Sjælland (Zealand, Copenhagen) na jimbo la Swideni la Skåne (Scania, Malmö), Barabara ya Strandvejen, Kaskazini ya ‘Indre By’, katika nyumba ya mpelelezi wa Tume ya Dunia aliyefundishwa na makomandoo wa SAS wa Uingereza Frederik Morgens.

Mpelelezi wa Tume ya Dunia Frederik Mogens ana nyumba mbili katika jiji la Copenhagen. Moja iko kaskazini-magharibi mwa Copenhagen katika kitongoji cha Norrebro; na nyingine Hellerup, kaskazini mwa Copenhagen. Norrebro ni nyumba yake rasmi ya familia aliyojenga yeye, wakati Hellerup ni nyumba yake ya siri aliyojengewa na Tume ya Dunia. Nyumba ya siri ya Mogens ni nyumba ya kisasa yenye mandhari nzuri ya kuvutia hasa sebuleni; kulikonakshiwa kwa televisheni na simu, jokofu dogo, mapambo ya wanyama, michoro ya rangi ya wasanii wa kale kama Pablo Picasso na Christoffer Eckersberg, na makochi makubwa ya Hans Wegner. Mipango yote ya Operesheni Kimbunga ilifanyika katika nyumba hiyo ya ghorofa: kabla ya Vijana wa Tume kwenda Roskilde (uwanja wa ndege wa Copenhagen) kupanda Grumman ya tume, kuelekea Guadalajara nchini Meksiko.

1 comment:

  1. Hapo ndipo ilipo nyumba ya siri ya mpelelezi wa Tume ya Dunia Sajini Frederik Mogens kutoka Denmaki.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...