Friday, 13 October 2017

Jiji la Jerusalem

Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli (Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.

Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Israeli Daniel Yehuda Ben-Asher Ebenezer, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Jerusalem, na mke wake mrembo Hadara na mtoto wake mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na Rais wa Tume ya Dunia.

Yehuda aliondoka usiku huo kwenda Yangon, Myama, ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo hayo, Nanda alimkabidhi Yehuda kachero wa Kolonia Santita Mandi Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya jiji la Yangon.

Baada ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake walikabidhiwa Operation Devil Cross, operesheni ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote.

Yehuda alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi Santana! Kwa sababu hiyo, sauti na picha ya Yehuda vilichukuliwa, watu wengi walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...