Thursday, 12 October 2017

Maamuzi Makali Dhidi ya Wenzetu

Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa? Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.

Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45).

Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.

Usilaumu, usilipize kisasi, usilaani, usihukumu, wala usitoe adhabu, lakini kuwa makini sana na maamuzi yako.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...