Kolonia Santita ni shirika la madawa ya kulevya (drug cartel). Panthera Tigrisi ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya, katili kuliko wote katika Hemisifia ya Magharibi. Kitabu hiki kinahusu ujasusi,madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa. Ukianza kukisoma hutakiweka chini kamwe unless kimeisha.
Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, World Drugs Enforcement Commission (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14 (lote) katika nchi za Hemisifia ya Magharibi - na duniani kwa jumla.
Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda - na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili - na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.
Kwa habari zaidi wasiliana na Enock Maregesi kupitia ukurasa wake wa Facebook: 
Kinapatikana Amazon na Authorhouse.com
“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.” - www.goodreads.com

No comments:
Post a Comment