Saturday, 26 November 2016

Matendo ya Mtu

Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua. Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.  

Tamthilia za Kiingereza na Kihindi zinazoonyeshwa hapa Tanzania watu wengi huzielewa ilhali hawajui Kiingereza wala Kihindi. Kwa nini? Kwa sababu wako makini na matendo ya wahusika.

3 comments:

  1. Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.

    ReplyDelete
  2. Nukuu hii inahusu zile tabia za ndani kabisa ambazo aghalabu watu huwa hawataki kuzionyesha kwa sababu za kinafiki. Si kila tabia. Tabia zingine ni za kuzidharau. Mtu akikuonyesha tabia yake ya ndani kabisa itakayoweza hata kukushtua wewe, tabia ambayo hajawahi kuionyesha hata mara moja, kuwa makini naye. Kwa sababu anayajua maisha yake kuliko wewe unavyoyajua.

    ReplyDelete
  3. Mtu hajawahi kuwa mwizi lakini leo kaiba, na umejua kwamba kaiba, amini kwamba ni mwizi.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...