201. Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!
Shetani anajua kwamba sisi ni warithi wa wokovu na kwamba dunia hii 
ni kitu kilichoahidiwa kwa Ibrahimu na watoto wake. Sisi wote ni watoto 
wa Ibrahimu. Anajua kabisa kwamba baadaye sisi ndiyo tutakaokuwa 
watawala halisi wa dunia hii. Hivyo, anajitahidi kwa kadiri ya uwezo 
wake wote ili hilo lisitokee. Shetani na malaika wake ni wengi sana, na 
wanatumia kila silaha waliyokuwa nayo kutawala dunia.
Inavyoonekana,
 kadiri mtu anavyozidi kupata elimu ndivyo anavyozidi kudharau uwepo wa 
Shetani na uwepo wa Mungu pia. Lakini, kwa upande mwingine, ndivyo 
anavyoonekana hajasoma sana na ndivyo Shetani anavyozidi kulaumiwa kwa 
kila dhambi inayotendeka. Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya kidini.
 Huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidunia, kwa sababu Shetani anajua 
ukiipata elimu hiyo hutajua kama yupo; na huwezi kutawala dunia bila 
elimu ya kidini, kwa sababu Mungu anajua ukiipata elimu hiyo utajua kama
 yupo. Hivyo, utamdharau Mungu ukipata elimu ya kidunia, utamheshimu 
Mungu ukipata elimu ya kidini.
Kama Shetani anatumia elimu 
kutawala dunia kama vile Mungu anavyotumia elimu kutawala dunia, nani 
alisema kuwa baadhi ya wasanii wa ‘Bongo Movie’ na ‘Bongo Flava’ ni 
wanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru? Je, wana 
elimu? Jibu unalo.
Anayesema fulani ni mwanachama wa chama cha 
siri cha kusaidiana cha wajenzi huru ana hakika? Haya mambo ni siri. 
Amejuaje? Kumbuka, usiamini, jua.
Kama wana elimu wanaweza kuwa wajenzi huru; lakini kama hawana elimu, hawawezi kuwa wajenzi huru.
Shetani
 ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya 
mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana 
kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila 
watu kujua.
Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye
 hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali 
kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile 
tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili 
akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. 
Ukitaka asikupumbaze, pokea roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea roho 
ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Usipoangalia kwa undani sana, Shetani anatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kumwona. Aidha, anaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani hataki tujue kama anatudanganya au ameshatudanganya tayari, na hataki tujue kama yuko hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.
ReplyDelete