Sunday 25 June 2017

Zona Rosa, Juárez, Mexico City

Zona Rosa, Juárez, Mexico City, ndipo yalipo Makao Makuu ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini Meksiko na katika nchi za Latino.
 
Zona Rosa (Kanda ya Pinki) ndipo shughuli zote za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya jijini Mexico City zinapofanyika, na ndipo ofisi ya Kamishna wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia Profesa Randall Buchanan Ortega ilipo. Ni kitongoji cha matajiri na ofisi (zikiwemo ofisi za kimataifa) magharibi mwa kitovu cha kihistoria cha Mexico City cha Centro Histórico. Hujulikana kwa kuwa na raia wengi wa Korea, kwa maduka, kwa starehe na kwa mashoga, mitaa yake mingi ikiwa na majina ya heshima ya miji ya bara la Ulaya.
 
WODEC Mexico City (Ofisi ya Tume ya Dunia) iko katika kona ya kusini ya Zona Rosa, karibu na Kituo cha Metro cha Insurgentes, na Barabara Kuu ya Chapultepec. Zona Rosa ni sawa na Posta Mpya kwa Dar es Salaam hapa kwetu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...