Monday 26 June 2017

Msaidie Katika Mungu

231. Mtu akikuomba msaada, mpe Mungu amsaidie.

Mtu akikuomba msaada, lakini una mashaka naye, hata kama huna mashaka naye, na una uwezo wa kumsaidia, usimsaidie wewe, mpe Mungu amsaidie, mpe kwa niaba ya Mungu. Uombee kimoyomoyo au vyovyote vile msaada huo kabla ya kumpa. Mungu mwenyewe atakuongoza ili umpe au usimpe. Kwani huyo anayekuomba anaweza kuwa malaika na anaweza kuwa Shetani hali kadhalika.

Mtu akikuomba msaada msaidie katika Mungu.

1 comment:

  1. Kama ni malaika, ukimsaidia umefanya jambo jema. Kama ni Shetani, Mungu atakulipia.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...