Vesterbrogade, Vesterbro, Copenhagen, Denmaki. Makao Makuu ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (WODEC) na Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani (WODEA).
Kuzunguka jengo la WODEC na mitaa yote ya jirani na WODEA kama Absalongade, Vaerdamesvej na mtaa wa makahaba wa Istedgade, Kolonia Santita walishatapakaa wakijitahidi kwa mbinu zao zote kujua nini kilifanyika katika chumba cha usalama cha CUTD.
Kolonia Santita walijua mienendo karibu yote ya wajumbe wa Kikao cha Dharura, na watumishi wengine wa Tume ya Dunia, kama malazi, mizunguko yao ya hapa na pale mpaka taratibu za usafiri za makamishna wa tume. Ujasusi huo uliwaletea Vijana wa Tume matatizo makubwa.
No comments:
Post a Comment