Friday, 30 June 2017

Simama Nyuma ya Maneno Yako

Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake yote. Fanya kile ulichosema utafanya, hata kama sehemu ya kile ulichosema utafanya uliinukuu kutoka kwa wengine, hata kama watu hawatakubaliana na wewe.

Simama nyuma ya maneno uliyoyasema mara mbili: kichwani na mdomoni mwako. Simama nyuma ya maneno uliyoyasema kwa hekima. Usiyumbe hata mambo yatakapokwenda segemnege.

Ukila kiapo fanya kile ulichoahidi katika kiapo, si kinyume chake hata kidogo, hata kama dunia haitakubaliana na wewe.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...