Monday, 3 July 2017

Kiongozi Aliyeteuliwa na Mungu


232. Kiongozi aliyeteuliwa na Mungu lazima aishi, afanye kazi, na atawale kulingana na jinsi alivyopangiwa na Mungu. Majukumu yake yatakuwa na changamoto nyingi, lakini changamoto hizo hazitamchanganya, kutokana na mambo kuwa mengi kichwani mwake. Wala ofisi yake haitamchanganya akili, kwa sababu Mungu ameshaiweka wakfu. Licha ya kuwa na nguvu kubwa ya kimadaraka atawatumikia watu kwa unyenyekevu, kuonyesha kuwa hakuna mamlaka ya matusi katika uendeshaji wa majukumu yake. Atafaa katika maeneo yote ya maisha.

Kiongozi bora hana upendeleo. Kwa maskini yupo, kwa matajiri yupo, kwa wanyonge yupo, kwa wababe yupo, kwa haki za wanawake yupo, kwa haki za watoto yupo, kwa wafanyabiashara yupo, kwa wafugaji yupo, kwa wakulima yupo, kwa wafanyakazi yupo. Hatapendelea upande wowote.

Kama wana wa wafalme wanavyotayarishwa kuwa viongozi baadaye, ndivyo Mungu anavyomtayarisha mtu kuwa kiongozi baadaye.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...