Monday 10 July 2017

Mungu Hatatusaidia Kwa Jambo Lolote Lile Analoona Halina Manufaa Kwa Wokovu Wetu

233. Mungu hatatusaidia kwa jambo lolote lile analoona halina manufaa kwa wokovu wetu. Atafanya kila linalowezekana ili tuishi kama anavyoishi yeye, na kama itamlazimu kutupa taabu za kila aina maishani, atafanya hivyo kwa sababu anatupenda.

Mungu yuko na sisi bado katika kiganja cha mkono wake, bado sisi ni hazina yake maalumu, bado sisi ni segula, lakini hilo halimzuii kutuadabisha tunapokwenda kinyume na mapenzi yake. Mungu anajua jinsi ya kuzalisha watoto bora, na wakati mwingine adhabu kali zaidi huzalisha matokeo ambayo ni bora zaidi. Kama anaona yule aliyepewa adhabu atashirikiana naye na atajifunza jambo kutokana na adhabu hiyo, yuko tayari kuishi naye.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...