Tuesday, 14 March 2017

Air France Flight 279

Ndege ya Murphy (Air France Flight 279 Boeing 747-400) ilinyanyuka Charles de Gaulle saa nne asubuhi kuelekea Copenhagen lakini ikalipuka na kuanguka Sittard, Limburg, Uholanzi; na Selfkant, Heinsburg, Westphalia ya Rhine ya Kaskazini, Ujerumani; na kuua watu wote – maili 215 kutoka Paris.

Hadithi ya Kolonia Santita ni ya kubuni haina uhusiano wowote na uhalisia isipokuwa maeneo na baadhi ya taasisi za kimataifa. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle ulikuwa umedhibitiwa vikali na CS-Paris (Tawi la Kolonia Santita Ufaransa na nchi zote za Ulaya ya Magharibi) wakati ndege ya Murphy inatua na kuondoka uwanjani hapo.

Ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, Air France Flight 279 Boeing 747-400, ndege ya Murphy, mara tu baada ya kukaa sawa angani futi 31,000 juu ya usawa wa bahari, mara tu baada ya rubani kuwasiliana na wenzake waongoza ndege akiwajulisha kuwa sasa alishakaa vizuri angani na waongoza ndege kumpa ruhusa ya kutambulika na kusafiri salama, ililipuka kwa kishindo kikubwa na kuanza kushuka kwa mwendo mkali kama risasi ya marisau.

Chini, katika mji wa Sittard, watu walikuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida, vipande vya ndege vilipojibamiza kwenye ardhi na kuacha shimo kubwa lenye ujazo wa tani 1500 za udongo na mawe! Vipande vya ndege vilisambaa (vikiwa hewani) katika eneo kubwa kama jiji la Dar es Salaam, zaidi ya kilomita za mraba 1500, na kukata mawasiliano yote ya simu na faksi katika eneo lote la kusini mwa Uholanzi.

Zaidi ya polisi 1000 na wanajeshi 600 walizagaa katika eneo la ajali (‘epicenter’) na bila kuchelewa wataalamu wakahitimisha ya kuwa Air France 279 ililipuka ikiwa angani, kabla hata haijafika chini. Watu 7 kutoka Sittard walikufa, pamoja na watu 304 (wote) waliokuwemo ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa.

Redio iliyotumika kuangusha ndege ya Murphy (Toshiba RT-SF 16) ilikuwa na mtambo maalumu wa saa na bomu, lililokuwa na nusu kilo ya baruti, lililotegeshwa kulipuka kwa muda na mwinuko maalumu juu ya usawa wa bahari.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...