Monday, 13 March 2017

2 + 2 = 5


216. Akili ya peke yako haina maana. 2 + 2 = 5.

Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Umoja una sisi (ubinadamu) si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu moja au kama mtu binafsi, kujenga shule ya kijiji, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa nyumbani au wa kampuni au wa nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika jambo lolote lile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.

Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...