Kufungwa kwa kosa ambalo hukufanya ni usaliti wa hali ya juu mno wa serikali dhidi ya yule aliyefungwa na dhidi ya familia yake hasa watoto kama anao. Serikali inadhani haina makosa na inatumia fedha nyingi kuwafunga watu. Pigana na serikali dhidi ya kesi yako, hata kama huna pesa, ndiyo maana kuna haki za binadamu, kama kweli umeonewa.
Serikali iwaombe radhi, tena mbele ya umma, watu waliofungwa kwa kuonewa halafu baadaye sheria ikathibitisha kuwa hawakuwa na hatia, ili waweze tena kuaminiwa katika jamii, na kuwalipa fidia, japo kidogo, ili waweze tena kuyaweka sawa maisha yao katika jamii.
No comments:
Post a Comment