Tupo watu takriban bilioni saba katika dunia hii. Kila mtu ni wa kipekee. Mathalani, wewe ni tofauti na baba yako au mama yako au mtu mwingine yoyote yule. Kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Kila mtu ana nafasi ya kwake mwenyewe aliyopangiwa na Mungu hapa duniani. Haijalishi wewe ni mwanamke au mwanamume, mweupe au mweusi, mfupi au mrefu, mzuri au mbaya, una nafasi katika nchi na dunia hii.
Unachotakiwa kufanya ni kuamka, kufumbua macho na kuujua ukweli. Tafuta maarifa katika Biblia kama wewe ni Mkristo. Tafuta maarifa katika Kurani kama wewe ni Mwislamu. Tafuta maarifa katika Yoga kama wewe haumwamini Mungu. Ukishaamka na kuujua ukweli, ukishapata nafasi katika nchi yako, kuwa kiongozi na mkarimu kwa wenzako. Jifunze kutoka kwa wengine ndani na nje ya tasnia yako. Usiwe mchoyo wa maarifa. Kuwa mwadilifu. Ukifanya hivyo utafanikiwa zaidi, utaipa heshima tasnia yako, na utaacha alama katika dunia baada ya kuondoka. Kuacha alama katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuacha alama katika dunia acha alama katika nchi yako.
Maarifa unayoyatafuta katika Biblia, Kurani au Yoga (‘Oriental Yoga’: ‘esoteric knowledge’: maarifa ya kujua siri ya uumbaji wa Mungu ya ‘Kabbalah’ ya Kiyahudi au ‘Kalachakra’ ya Kibudha ya bara la Asia; siri ya sayansi ya kurefusha maisha ya mafundisho ya kiroho ya ‘Arcanum’ ya Misri au Kemia ya Mungu au ‘Alchemy’; mafundisho ya kiroho ya ‘Rosicrucia’ ya bara la Ulaya tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nne; ‘sex magic’, ‘sex magic’ inaweza kukupa utajiri au umaskini hivyo kuwa makini, n.k.) ni hekima na busara. Vingine vyote vitajileta vyenyewe.
‘Kabbalah’ ni sayansi ya Mti wa Uzima wa Milele wa Bustani ya Edeni au ‘The Tree of Life of the Garden of Eden’ katika mbingu ya nne, ambayo ni ramani ya ulimwengu na roho ya mwanadamu; au Sayansi ya Mungu, uchawi wa kujua 99% ya siri ya uumbaji wa Mungu.
Tafuta kitu cha kufanya katika maisha yako unachokiamini zaidi kuliko pesa, kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika kwa mfano, na ukishakipata kuwa kiongozi na mkarimu kwa wengine. Kutoa sauti kwa ajili ya watu wasioweza kusikika inaweza kuwa ndiyo nafasi yako uliyopangiwa na Mungu uitumie kwa manufaa ya wengine, si kwa manufaa yako, nafasi za wengine zitatumika kwa manufaa yako. Kuna vitu vingi ambavyo mtu anaweza kufanya; chagua kimoja kinacholeta maana zaidi katika maisha yako na ukifanye hicho, kwa nguvu zako zote.
Maarifa unayoyatafuta katika Biblia, Kurani au Yoga ni hekima na busara.
ReplyDelete