Msitu
wa Mvua wa Amazoni nchini Kolombia – na nchi zingine nane za kaskazini
mwa bara la Amerika ya Kusini huko ‘Americas’ – magaidi wa Kolonia
Santita walipokuwa wameficha tani 600 za madawa ya kulevya chini ya
uangalizi wa waasi wa kisiasa wa Kolombia, Peru, Brazili, Venezuela na
Bolivia, kabla ya kuzihamishia nchini Meksiko kwa ajili ya usambazaji wa
dunia nzima.
Ndani ya kitabu cha Kolonia Santita mtu mwenye historia kubwa na Msitu wa Amazoni ni Nicolas Kahima Kankiriho. Kankiriho alikuwa askari mamluki wa Uganda aliyetoroka na El Tigre katika nyambizi ya Jefe de Jefes SPD (‘the Silent Predator of the Deep’),
iliyotengenezwa na Belinsky, katika Ghuba ya Meksiko Septemba 16, 1986.
Msitu wa Amazoni ndiyo uliyomkuza Kankiriho, na ndiyo uliyompatia kazi
kama mlinzi binafsi wa kiongozi wa Kolonia Santita.
Msitu
wa Amazoni ni msitu mkubwa kuliko misitu yote ya mvua ulimwenguni,
wenye ukubwa wa kilometa za mraba milioni 5.5 (maili za mraba milioni
2.123), uliotapakaa katika nchi tisa za Amerika ya kusini; ikiwemo
Bolivia, Venezuela, Brazili, Peru, na Kolombia.
No comments:
Post a Comment