Wednesday, 8 February 2017

Vita ya Madawa ya Kulevya si Vita Ndogo

Vita ya madawa ya kulevya si vita ndogo. Biashara hii ina laana! Kadiri unavyoipiga vita ndivyo inavyoshamiri. Lakini Mungu ni mkubwa. Kama umeamua kuipigana vita hii pigana, hata mwisho wa maisha yako.

Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.

Serikali ishirikiane vizuri na wananchi. Ijenge uaminifu kati yake na wananchi. Wananchi wana siri nyingi. Serikali ikijenga urafiki na wananchi, wananchi watajenga urafiki na serikali. Halafu kazi ya serikali itakuwa rahisi, na wananchi watakuwa wameitumikia serikali.

Kila mtu anajua kwamba Gilberto Orejuela alikuwa kipenzi cha wananchi wa Cali huko Kolombia kwa sababu alikuwa rafiki yao. Pablo Escobar alikuwa kipenzi cha wananchi wa Medellín kwa sababu alijichukulia jukumu la serikali kwa Medellín na kwa miji mingine yote ya Kolombia kwa jumla. Hata Joaquín Archivaldo Guzmán Loera ‘El Chapo’ wa Meksiko alifanikiwa sana kwa sababu alikuwa karibu mno na wananchi wa Sinaloa.

Mamafia wa Amerika ya Kusini na Kaskazini wanafanikiwa kwa sababu wanajenga urafiki na wananchi. Serikali ikitaka kufanikiwa ijenge urafiki na wananchi.

Watu walioathirika na madawa ya kulevya ni wa kuonea huruma. Hawana uwezo wa kuachana na kingwagu cha madawa ya kulevya kwa nguvu zao wenyewe. Wakulima na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya hawana huruma.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...