Thursday, 9 February 2017

Mashabiki

Maadui ni wazuri kuliko marafiki na mashabiki ni wazuri kuliko maadui. Maadui wanakusaidia kujua wewe ni nani na kwa nini uko hapa. Ukishajua wewe ni nani na kwa nini uko hapa, hakuna mtu atakayekuzuia kufanya chochote unachokiamini zaidi na kukifanya. Chochote unachokiamini zaidi na kukifanya ndicho Mungu alichokupangia kufanya hapa duniani, na kwa sababu hiyo utapata maadui. Ili utoke lazima uwe na mashabiki, marafiki na maadui.

Marafiki wanaweza kukupotosha bila wao wenyewe kujua na bila kuwa na nia mbaya ya aina yoyote ile; na wanaweza kuwa washauri wazuri kwa sababu wanakujua vizuri unapokuwa na huzuni, na wanakujua vizuri unapokuwa na furaha pia. Kwa mfano; rafiki yako anaweza kukushauri kusomea uhasibu wakati Mungu amekupangia utawala, au anaweza kujua aongee na wewe wakati gani kulingana na tabia yako ya kubadilikabadilika. Maadui wanasaidia kujua kipaji ulichopewa na Mungu – ukifanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako halafu ukawa na maadui ujue hicho ndicho Mungu alichokupangia kufanya, hivyo usikate tamaa – na mashabiki wanasaidia kufanya kipaji chako kiwe na uhai.

Ukitaka kuwa na mashabiki fanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako, kila siku.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...