WODEA (‘World Drugs Enforcement Administration’) ni shirika la
kujitegemea la kimataifa – linalofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa
Mataifa – lenye nia/shabaha ya kukomesha (katika dunia) madawa haramu ya
kulevya, ya madaraja yote, pamoja na ugaidi wa kimataifa wa aina zote –
hasa wa kimadawa, kisiasa na kinyukilia; kwa ajili ya amani, afya na
usalama wa kimataifa.
WODEA ilianzishwa chini ya Mkataba wa
Kisheria wa Kimataifa wa WODEA (‘WODEA Statute’) uliosimamiwa kwa
kipindi cha siku tatu mfululizo na Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, UNSC, Novemba 1975. Tofauti na Shirika la Kimataifa la Nishati
ya Nyukilia, IAEA, ambalo huwajibika kwa UNSC na kwa Mkutano Mkuu wa
Umoja wa Mataifa; WODEA huwajibika kwa UNSC na kwa Baraza la Uchumi na
Ustawi wa Jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC.
WODEC, Chombo Kikuu
cha WODEA, ambayo hutumika kama kongamano la majadiliano ya masuala ya
madawa na ugaidi ya kimataifa; huundwa na vyombo vingine vidogo vitatu:
Bodi ya Makamishna ya Tume ya Dunia (WBC – ‘WODEC Board of
Commissioners’), Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia (WGC – ‘WODEC General
Conference’) na Sekretarieti ya Tume ya Dunia. WBC ni Chombo cha Sera
cha Tume ya Dunia. Kina wajumbe 12 wanaoteuliwa na Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa, na 26 wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia.
Wajumbe 12 (watano wa kudumu wa UNSC na saba viongozi wa kanda za
WODEA) huteuliwa na UNSC kwa kipindi cha miaka mitano, wakati 26
huchaguliwa na WGC kwa kipindi kimoja cha miaka miwili. WBC hutoa
mapendekezo kwa WGC kuhusu bajeti na shughuli zote za WODEA.
Rais wa WODEA huchaguliwa na WGC kwa mapendekezo ya UNSC. WBC
hupendekeza majina sita kwa UNSC ambayo huchagua majina matatu kati ya
hayo sita na kuyapeleka katika Mkutano Mkuu wa WODEA – kupigiwa kura ya
Kamishna Mkuu wa WODEC na Rais wa WODEA kwa kipindi cha miaka mitano.
Kamishna Mkuu wa WODEC ni Rais wa WODEA. Wakati WBC hukutana mara nne
kwa mwaka mjini Copenhagen kuanzia Novemba, WGC (nchi wanachama 143)
hukutana mara moja kwa mwaka katika mwezi wa Novemba kuidhinisha bajeti
na mapendekezo ya WBC – kwa ajili ya Sekretarieti ya Tume ya Dunia.
Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika na utekelezaji wa mapendekezo
yote yaliyopitishwa na WBC na WGC kwa niaba ya WODEA. Huchaguliwa na WBC
na kuidhinishwa na WGC kwa kipindi cha marudio cha miaka mitano.
Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika pia na nguvukazi ya watu zaidi
ya 7,000 duniani kote na bajeti ya wastani wa dola za Kimarekani milioni
400 kwa mwaka mzima.
Mbali na WBC, WGC na Sekretarieti ya Tume
ya Dunia, WODEC ina vyombo vikubwa vitatu vya dola: Idara ya Polisi ya
Tume ya Dunia (WPD), Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS) na Kikosi
Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC). EAC iliundwa kwa
makubaliano maalumu ya Azimio la Copenhagen kati ya WODEA na Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa – Novemba 1980.
WODEC ina maabara
tatu za kikemia, ofisi tatu za mahusiano mema (Vienna, Pretoria na New
York), kliniki saba za madawa ya kulevya na kanda sita katika mabara
sita ya dunia nzima. Kila kanda ina bodi ya wakurugenzi, idara ya
polisi, usalama, sekretarieti, maabara na kliniki za madawa ya kulevya.
Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia huanzia Somalia mpaka
Kameruni mpaka Afrika Kusini. Kanda ya Afrika ya Kaskazini ya Tume ya
Dunia huanzia Eritirea mpaka Nijeria mpaka Tunisia, isipokuwa Moroko
ambayo iko katika kanda ya Ulaya.
“Kama viongozi wenu wa kanda
walivyowahabarisha tuna kazi kubwa mbele yetu inayohitaji moyo mkubwa wa
kujitolea na ujasiri wa hali ya juu kujaribu tu hata kuifanya. Kazi ya
Tume ya Dunia ni kupambana na aina yoyote ya uhalifu wa madawa ya
kulevya kwa makusudi kutetea afya na amani ya dunia yote kwa watu wote
ulimwenguni. Hii ni vita tuliyokula kiapo sisi wote kuipigana – vita ya
sheria na udhalimu, wa madawa ya kulevya, na ugaidi wa kimataifa,
tutakayopigana mpaka sheria ishinde na kufuata mkondo wake.” – Boidin
Tony Versnick (Rais, Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, 1985 –
1992)
Watu wananiuliza: “Je, Paul Makonda atashinda vita ya
madawa ya kulevya katika mkoa wake bila kufuata mfumo wa Tume ya Dunia
ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya?” Jibu lake ni ndiyo na hapana. Hapana
kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye anayejua. Ndiyo kwa sababu Makonda ana
ulinzi.
Paul Makonda ataweza kushinda vita ya madawa ya kulevya
kwa sababu rais na waziri mkuu hawajihusishi na madawa ya kulevya. Nao
watamlinda kwa gharama yoyote.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
anaposema vita hii iwe ya wazi na ya kila mtu wakati yeye ana ulinzi
wengine watalindwa na nani? Vita dhidi ya madawa ya kulevya inapaswa
kupiganwa kiintelijensia zaidi kuliko kipolisi, kisiasa, au sifa
binafsi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, saa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safi...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
WODEA is a fictional independent international agency; employed by the United Nations to bring peace, security and prosperity to the world by fighting illegal drugs; and narco, political and nuclear terrorism.
ReplyDelete