Friday, 10 February 2017

Museo Nacional de Culturas Populares

Jumba la Makumbusho la Taifa la Utamaduni wa Kileo, ‘Museo Nacional de Culturas Populares’, la Meksiko, lililoko Coyoacán jijini Mexico City, Vijana wa Tume pamoja na mtoto wa rais wa Meksiko (Debbie) walipofukuzana na magari ya magaidi na magari ya polisi; kutoka katika ‘hacienda’ ya Panthera Tigrisi ya Coyoacán, mpaka karibu na nyumba ya siri ya Vijana wa Tume ya Cuauhtémoc (‘Kwauteimak’).

Polisi wa kituo cha kati cha Coyoacán kumbe hawakuwa mbali sana na Jumba la Makumbusho la Taifa la Utamaduni wa Kileo la ‘Museo Nacional de Culturas Populares’ la Coyoacán. Walipoona magari yakifukuzana waliona ujanja ni kuwakatisha Vijana wa Tume katika vichochoro. Haikuchukua muda magari sita ya polisi yalitokeza Vallarta (Barabara ya Vallarta) na kuliona gari la Vijana wa Tume Gómez Farías likipepea kwa mwendo mkali kuelekea Cuauhtémoc, na magari ya magaidi kwa nyuma yao. Kwa vile Ferrari ilikuwa mbali kidogo na magari ya magaidi, polisi hawakuitilia maanani sana kwa kudhani yale mawili (ya magaidi) ndiyo yaliyokuwa yakifukuzana. Bila kuchelewa, magari mawili ya polisi yalikamata Hidalgo na kuzunguka mpaka Moctezuma halafu yakasimama ghafla katikati ya Moctezuma na Gómez Farías – katikati ya magari mawili ya magaidi na gari la Vijana wa Tume. Wakati huohuo magari mengine (manne) ya polisi yakitokea Mtaa wa Vallarta nayo yakasimama nyuma ya magari ya magaidi; hivyo kufanya magari ya magaidi yawe katikati ya magari ya polisi, na polisi wakaisahau Ferrari ya Lisa.

Vijana wa Tume walichekelea sana katika Ferrari ya Lisa huku wakiushukuru mno uongozi wa Polisi wa Coyoacán. Walikuwa na uwezo wa kusimama na kujitambulisha lakini hawakuwa na muda wa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...