Wednesday, 8 February 2017

Wasifu wa Viongozi wa Kolonia Santita ni Siri

Kuna sababu ya msingi inayoleta tofauti kati ya madaraja ya mafanikio miongoni mwa maazimio ya watu. Sababu hiyo ni mazoea ya utunzaji wa siri. Zipo sababu nyingi zinazofanya watu wenye uwezo wa kutunza siri wafanikiwe zaidi kuliko watu wasiokuwa na uwezo wa kutunza siri. Hiki ni kitu ambacho watu wengi hawakijui. Unapotambua sababu ya siri kuwezesha mafanikio ya maazimio ya watu, unaweza kuwa na uwezo au weledi wa kutosha juu ya mafanikio yako.
 

Viongozi wa Kolonia Santita walifanya kazi katika mazingira ya siri kubwa. Bila hivyo wangeshakamatwa. Hata wale viongozi wa serikali waliokuwemo ndani ya Mpango wa Fadhila ya Uhalifu wa Kolonia Santita na Serikali ya Meksiko, mpango wa viongozi wa serikali ya Meksiko kuwasaidia wahalifu pindi wanapoanguka katika mikono ya sheria na kutetea shughuli zao zote za kihalifu kwa malipo ya bima ya utekaji nyara ya familia zao, wangeshakamatwa pia.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...