Monday, 13 February 2017

Pombe

212. Pombe haina adabu. Ukilewa unakuwa mtoto tena.

Kidini kufananishwa na mtoto ni sifa nzuri kwani ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya watu kama wao. Lakini kidunia si!

Ukiitwa mtoto kidini ina maana una imani na unyenyekevu mbele ya Mungu, kama ambavyo mtoto ana imani na unyenyekevu mbele ya mzazi wake. Lakini ukiitwa mtoto kidunia watu watakudharau.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...