Sunday, 12 February 2017

Machine Pistol Model 5

Bunduki iliyotaka kumuua Mpelelezi wa Tume ya Dunia John Murphy Ambilikile huko Mexico City, MP5, iliyomuua Kiongozi wa CS-Copenhagen Regner Steiner Valkendorff huko San Antonio, Murphy alipokamatwa na Kolonia Santita baada ya kuiba kitabu cha siri katika makao makuu ya Kolonia Santita ya San Ángel.

MP5 (‘Maschinenpistole 5’, au ‘Machine Pistol Model 5’) ni mojawapo ya bunduki hatari zilizotengenezwa na Kiwanda cha Silaha cha Heckler & Koch GmbH cha Ujerumani; zilizotumiwa na makomandoo wa Tume ya Dunia na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Kolonia Santita na dhidi ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kwa mpangilio huo. MP5 ina uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja risasi 100 katika chemba yake ya ‘century’, kupiga risasi 900 kwa dakika (kwa kutumia mkanda wa risasi), na kufyatua risasi kwa kiasi cha kuleta maafa makubwa katika umbali wa meta 200 au futi 656. Mnamo mwaka 1980 katika Operation Nimrod ya Jeshi la Uingereza, MP5 ilijipatia umaarufu mkubwa duniani katika Ubalozi wa Irani huko Kensington jijini London; ilipotumiwa kwa mafanikio makubwa na makomandoo wa SAS, kuokoa mateka 26 dhidi ya magaidi 6 wenye msimamo mkali wa Irani, katika tukio lililoonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...