Tuesday 14 February 2017

Bentley Continental S


Bentley Continental S, gari la kifahari lililotumiwa na majambazi wa Kolonia Santita nchini Urusi (CS-Moscow) kumteka nyara Mpelelezi wa Tume ya Dunia John Murphy Ambilikile (Ambie) katika Mtaa wa Smolenskaya Prospekt mjini Moscow.

Bentley Continental S, gari la majambazi wa CS-Moscow (Tawi la Kolonia Santita Nchini Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki kama vile Belarusi, Moldova na Ukraini [na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini kama vile Masedonia, Montenegro, Uturuki na Ugiriki]); lilimfuata Murphy, Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Tanzania, kuanzia Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo mpaka Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol katikati ya Moscow, karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod: kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale, ambapo teksi ya Murphy ilipata matatizo. Lakini, Bentley iliendelea mbele huku wakihakikisha Murphy hawapotei na kusimama nje ya kioski mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy. Bentley (iliyokuwa na namba za usajili za kibabe, B 001 BB 77 RUS, za viongozi wa chama tawala mali ya mwanajeshi wa zamani wa ‘Red Army’ kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka) baadaye iliendelea kumfuatilia Murphy mpaka Smolenskaya Prospekt, walipomteka nyara halafu, wakaondoka kwa mwendo mkali bila hata kujali theluji mpaka Miklukho-Maklaya katika ‘dacha’ ya Kolonia Santita. Hapo walimtesa Murphy lakini akaokoka katika mazingira magumu ya kutatanisha.

John Murphy alitua katika Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II mjini Moscow, tarehe 1/11/1992, kutokea Dar, Cairo, Instanbul na Odessa chini Urusi. Hivyo, Murphy alifika Copenhagen tarehe 1/11/1992 badala ya tarehe 31/10/1992 kama ofisi ya usalama ya tume ilivyomtegemea. Pamoja na matatizo yote aliyoyapata Moscow, Murphy angekufa kinyama kama angefuata maelekezo ya WODEC-Intelligence.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...