AK-47 ya Panthera Tigrisi, aliyoipenda kuliko zote, ikiwa imehifadhiwa katika jumba la makumbusho la Tume ya Dunia mjini Mexico City.
AK-47 ni bunduki maarufu kuliko zote hapa duniani, na bunduki inayouzwa zaidi kuliko zote nchini Marekani baada ya AR-15. AK-47 ina uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja risasi 30 katika chemba yake, kupiga risasi 600 kwa dakika (kwa kutumia mkanda wa risasi), na kufyatua risasi kwa kiasi cha kuleta maafa makubwa katika umbali wa meta 365.76. Majambazi wa Kolonia Santita hupendelea sana bunduki za AK-47 kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufanya kazi, bei nafuu, na wingi wa kupatikana. Bunduki za Kalashnikova hutema risasi kama cherehani inavyoshona.
No comments:
Post a Comment