214. Umri sahihi wa kuoa au kuolewa kulingana na kanuni ya ndoa iitwayo ‘optimal stopping’ ni miaka 26. Kanuni hii ya hesabu hujulikana kama kanuni ya asilimia 37, welekeo wa 0.37 wa kumpata mwenza bora zaidi katika maisha yako kuliko wengine wote.
Masharti ya kanuni ya ndoa ya kuachana na ukapera yanakutaka uwe umeshatembea na kukataa asilimia 37 ya wapenzi wako katika kipindi chote cha maisha yako, ili kumpata mpenzi mmoja bora zaidi ambaye ndiye hasa utakayeoa au kuolewa naye.
Lakini kanuni hii ina walakini. Kwa mfano utajuaje watu au wapenzi utakaotembea nao au kuachana nao katika kipindi chote cha maisha yako? Au itakuaje kama mpenzi wako wa kwanza uliyemwacha ndiye yule ambaye Mungu alikupangia kuwa naye maishani?
Kama umeamua kuoa au kuolewa ukiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 40, kulingana na kanuni ya kuachana na ukapera, umri wa kuwa na msimamo kuhusiana na mtu utakayeoa au kuolewa naye ni baada tu ya kufikisha umri wa miaka 26. Kabla ya hapo kuna uwezekano ukakosa wachumba bora, baada ya hapo wachumba bora wanaweza kuanza kupotea, hivyo kukupunguzia uwezekano wa kumpata mke au mume aliye mwema.
Tovuti za miadi (‘dating sites’) hutumia ‘optimal stopping’ kuwachagulia watu wachumba wao. Wanachofanya ni kwamba wanachagua watu 100. Wanaondoa 37% ya kwanza ya wale ambao sifa zao haziendani na sifa unazozitaka. Kisha wanakuchagulia mtu waliyeona ni bora zaidi kuliko wote waliobakia. Huyo waliyekuchagulia anaweza kuwa mke au mume bora. Lakini Mungu ana mipango yake. Unaweza kushangaa mke au mume bora akatoka kwenye 37% ya wale walioachwa.
Mtu anaweza kusema ana wachumba sita ambao anafikiria kuchagua mmoja kuwa mke au mume. Akichagua kiholela atakuwa na hakika 9% ya kumpata mwenza bora wa maisha. Lakini akitumia ‘optimal stopping’ atakuwa na hakika 37%!
Kanuni hii inaweza kutumika katika uchaguzi wa kitu chochote kama vile nyumba, kazi, gari, na kadhalika.
ReplyDelete