Kuna siri ambayo wanaume hawaijui kuhusu wanawake. Wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili wana mapenzi ya kweli. Ishirini na mbili hadi ishirini na nne wana mawenge. Ishirini na nne hadi ishirini na saba wanajitambua. Ishirini na saba hadi thelathini wana hofu na mashaka mengi. Thelathini hadi thelathini na tano wana msongo wa mawazo. Thelathini na tano hadi arobaini na mbili ndoa nyingi huvunjika.
Kwa hiyo, kuwa makini na wanawake na wanaume hasa wanawake na wanaume wa kundi la sita. Wanawake na wanaume hasa wanawake na wanaume wa kundi la sita, wengi wao wana DNA ya wapenzi wao wa zamani.
Wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili wanaweza kutawaliwa. Ishirini na mbili hadi ishirini na nne wanaweza kukuumiza. Ishirini na nne hadi ishirini na saba unaweza kuweka malengo nao yenye natija. Ishirini na saba hadi thelathini watakuchunguza sana na hawatakupenda kutoka moyoni. Thelathini hadi thelathini na tano wamejawa na dharau za kijinga. Thelathini na tano hadi arobaini na mbili watakung’ang’ania kupoza hasira za huko walikotoka.
Tofauti na wanawake wenye umri wa miaka kumi na nane hadi ishirini na mbili, na wanawake wenye umri wa miaka ishirini na nne hadi ishirini na saba, wengine wote ni kubahatisha.
Mwanamke mwenye umri wa miaka arobaini na mbili na kuendelea anafaa kuolewa kama ni mjane na ataweza kuwapenda watoto wako kama mama yao alishafariki. Yule ambaye hajawahi kuolewa au aliyewahi kuolewa lakini akaachika bado ni kubahatisha, kwa sababu hujui kwa nini hajaolewa au kwa nini aliachika, hata kama ana watoto.
Hayo ni maneno ya wahusika wangu kwenye kitabu… Mhusika, takriban, ana uwezo wa kusema jambo lolote.
No comments:
Post a Comment