Sunday, 29 January 2017

Miwani ya Kipelelezi Aina ya Aviator

Miwani ya kipelelezi aina ya Aviator (MicroSD, 32GB, GLSun720P) – iliyotumiwa na makachero wa kike wa Kolonia Santita Giovanna Garcia, Delfina Moore, Amalia Gonzalez, Mandi Santana na Kamanda wa Makachero wa Kolonia Santita Sonia Padilla; kuwapeleleza Vijana wa Tume wa Executive Action Corps John Murphy, Radia Hosni, Daniel Yehuda na Frederik Mogens; Oktoba, 1992.

Kamishna Profesa Randall Ortega ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen Kastrup, kabla ya makamishna wengine. Ndege yake, Lufthansa, iliondoka saa 2:40 usiku kwenda Mexico City kupitia Dusseldorf na Frankhurt, Ujerumani. Murillo Montana alifika uwanjani hapo mapema na kuondoka saa 4:00 usiku na BA kwenda London, Miami, Lima, na Bolivia – mwisho wa safari yake. Wote, Ortega na Montana, ndani ya ndege zao, walikaa na wasichana warembo waliokuwa na safari sawa na za makamishna. Mmoja, aliyekaa na Ortega, alikuwa na safari ya Mexico City kupitia Dusseldorf na Frankfurt, Ujerumani – kama Kamishna Ortega. Na mwingine, aliyekaa na Montana, alikuwa na safari ya La Paz, Bolivia; kupitia London, Miami na Lima, Peru – kama Kamishna Montana. Wasichana hao walikuwa wakarimu, wazuri, wacheshi na wapenda watu – wote walivaa miwani myeusi.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...