Monday, 30 January 2017

Fidel Castro

210. Fidel Castro alitenda haki katika taifa lake ndiyo maana Mungu akamsaidia yeye na wananchi wake. Ijapokuwa ameondoka, lakini fikira zake sahihi zitaendelea kuwepo. Taifa la Kuba Mungu ataendelea kulibariki, kwa sababu fikira za Wakuba ni fikira za Fidel Castro.

Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahiki au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.

Yeyote yule anayepingana na mamlaka anapingana na kile ambacho Mungu alikianzisha mwenyewe, na wote wanaofanya hivyo watakiona cha mtema kuni. Kwani yule anayetawala ni mtumishi wa Mungu kwa ajili yako, haijalishi anatenda haki au anatumia mabavu. Watawala wana nguvu ili waitumie. Ni watumishi wa Mungu, mawakala wa Mungu kwa ajili ya kuwaadhibu watenda maovu. Tii sheria bila shuruti. Si tu kwa sababu ya kuogopa adhabu. Tii sheria bila shuruti kwa kudhamiria.

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...