Tuesday, 13 December 2016

‘The Grand Old of the City’

D'Angleterre. Hoteli ya kimataifa daraja la kwanza, ‘The grand old of the city’, nyota tano, katika kona ya mitaa ya Østergade na Kongens Nytorv katikati ya Copenhagen, mkabala na duka kubwa la kujihudumia mwenyewe la Magasin du Nord, Radia Hosni, mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Tunisia alipofikia.

Hoteli ya D’Angletere, karibu na sanamu la farasi la Mfalme Christian wa Nne na mkabala na duka la Magasin, katikati ya geti la mashariki la Copenhagen na Bandari ya Nyhavn, ndipo Tume ya Dunia ilipoandaa malazi ya siri ya mpelelezi wake mashuhuri Radia Hosni. Lakini, ndani ya saa moja tu, Kolonia Santita wakajua Hosni alipokuwa; na kuandaa njama kamambe za kumuua usiku huo.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...