Mpelelezi
 wa Tume ya Dunia kutoka Yerusalemu, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda 
Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha 
mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli 
(Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya 
Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama
 la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.
 
Daniel
 Yehuda, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Yerusalemu, na mke wake mrembo 
Hadara na mtoto wao mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku 
alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia
 U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na 
Rais wa Tume ya Dunia. Yehuda aliondoka usiku kwenda Yangon, Myama, 
ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi 
aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa 
kuyafuata, Yehuda alikabidhiwa na Nanda kachero wa Kolonia Santita Mandi
 Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) 
ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya Yangon. Baada 
ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake 
walikabidhiwa Operation Devil Cross, ya kung’oa mizizi ya Kolonia 
Santita duniani kote. 
Yehuda
 alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi 
Santana! Kwa sababu hiyo, picha na sauti yake vilichukuliwa, watu wengi 
walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City. 

No comments:
Post a Comment