205.
 Kiongozi kwa sababu ya haki akibarikiwa na Mungu, hata watu 
anaowaongoza watabarikiwa na Mungu pia. Lakini kama kiongozi amelaaniwa 
na Mungu kwa sababu ya uovu, hata watu anaowaongoza watalaaniwa pia. 
Wakati
 Yuda ikiongozwa na kiongozi mzuri na mwenye haki kama Yosia, taifa 
lilistawi. Lakini ilipokuwa chini ya mwovu Manase, taifa 
lilisambaratika. Katika karne hii, Uingereza ilipata msukosuko mkubwa 
mwaka 1936 juu ya uamuzi wa Edward VIII kuoa mwanamke wa Kimarekani 
aliyekuwa mtalaka Wallis Simpson. Uamuzi huo ulisababisha matatizo 
makubwa ya kikatiba, na nusura serikali ya Uingereza ijiuzuru. Hata 
hivyo, kaka yake mdogo, George VI, kwa mapenzi makubwa na nchi yake, 
huku akikataa katakata kuondoka London wakati wa Vita Kuu ya Pili ya 
Dunia, aliliongoza taifa hilo katika kipindi kigumu zaidi kuliko vyote 
katika historia ya Uingereza. Kanuni hii ya uongozi ina ukweli katika 
jambo lolote kubwa na hata dogo la ujasiri.
Katika
 maisha, kila mtu ni kiongozi na ni mfuasi pia kutegemeana na hali. 
Kiongozi hatakiwi kuwa na kiburi, wala hatakiwi kuwa na roho yenye 
kutakabari, roho ya jeuri na kuona wengine si kitu, kwa sababu kiburi na
 roho yenye kutakabari huleta maangamizi na maanguko makubwa katika 
jamii. Viongozi wa mataifa wana jukumu kubwa kwa sababu kama wataruhusu 
maadili yaanguke, nguvu zao zote za kijeshi na kiteknolojia 
hazitawasaidia. Sifa ya kwanza ya kiongozi ni kuwa na maadili mema. 

Kiongozi akiwa na maadili mema atatenda haki.
ReplyDelete