Thursday, 15 December 2016

Madawa ya Kulevya Yaliyotumika Katika Kitabu cha Kolonia Santita

Madawa ya kulevya yaliyotumika katika kitabu cha KOLONIA SANTITA: LAANA YA PANTHERA TIGRISI. Kokeini, tani 183. Heroini, tani 90. Methamfetamini, tani 81. Eksitasi, tani 27.54. Bangi, tani 186. Uyoga wa kichawi, tani 60.

Kolonia Santita ilikuwa na tani 627.54 za madawa ya kulevya ilizokuwa imezikusanya kwa siri kwa muda wa miezi 9 mfululizo. Ilikuwa imepanga kuzisafirisha ndani ya siku 10 baada ya kutokea kwa mauaji ya Tijuana-San Diego, katika mpaka wa Meksiko na Marekani; kwenda Asia, Afrika, Amerika, Ulaya na Australia, kabla ya kukamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani WODEA. Kokeini tani 183, heroini tani 90, methamfetamini tani 81, eksitasi tani 27.54 (vidonge milioni 110.16). Bangi tani 186, uyoga wa kichawi tani 60. Madawa hayo yalikuwa na thamani ya mtaani ya shilingi za Kitanzania trilioni 12.9.

Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.

2 comments:

  1. WODEA ni shirika mama la WODEC.

    ReplyDelete
  2. Vita dhidi ya madawa ya kulevya itakwisha iwapo serikali zitapambana na wakulima, wasafirishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa madawa ya kulevya kwa nguvu ya pamoja ya asilimia mia moja. Aidha biashara haramu ya madawa ya kulevya itakwisha iwapo mataifa yatafuata muundo wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (WODEC) ambapo kila kanda ina bodi ya wakurugenzi, sekretarieti, idara ya polisi, idara ya usalama, ofisi za mahusiano mema miongoni mwa mataifa, maabara, kliniki, nguvu kubwa ya dola, kikosi maalumu mbali na polisi kwa ajili ya mapapa wa madawa hayo, na programu za kufundisha wananchi faida na hasara za madawa ya kulevya.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...