Wednesday, 9 November 2016

Smolenskaya Prospekt

Smolenskaya Prospekt. Hapa ndipo ilipo Ofisi ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya Nchini Urusi, WODEC-Moscow, inayoongozwa na Dmitri Olegushka (tajiri) na Nikolay Narochnitskaya ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza nyambizi.

John Murphy alipotoka Teatralny Proezd (teksi yake iliposimama kutokana na matatizo ya injini), aliendelea kutembea mpaka Krasnaya Ploshchad (Uwanja Mwekundu au ‘Red Square’) – eneo la shughuli za kiserikali na kitovu cha biashara cha Moscow ya leo – ambapo ndipo utapata njia ya mkato kirahisi kuelekea WODEC. Mbele ya ‘Red Square’, Murphy alikamata barabara nyembamba ya kushoto na kuendelea kutembea kwa hasira; huku sasa akiziona ofisi za tume meta kama mia nne hivi mbele yake kushoto. Alipofika Smolenskaya Ploshchad (Uwanja wa Smolenskaya) kabla hajavuka barabara kuingia Smolenskaya Prospekt, katika ofisi za Tume ya Dunia, kitu ambacho Murphy alikitegemea kilitokea! Bentley, gari la magaidi, lilifunga breki ghafla. Watu watatu wakashuka, chapuchapu, na kumrusha Murphy ndani ya gari. Halafu wakaondoka, kwa mwendo mkali, bila kujali theluji, kuelekea Yugo Zapadnaya.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...