Tuesday, 22 November 2016

Mpelelezi wa Tume ya Dunia Radia Hosni

Eneo la kihistoria la mjini Tunis nchini Tunisia linalosifika kwa majengo mengi ya kale na mitaa mingi myembamba iliyoshonana, Medina, Mpelelezi wa Tume ya Dunia Radia Hosni alipomshusha mchumba wake Fathi Meoki – kipindi akielekea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Carthage (kutokea Uwanja wa Mpira wa El-Manzeh) kumpokea Bosi wa Kanda ya Afrika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia Hussein Kashoggi.

Ijumaa, Radia alikuwa na ratiba ya kumpokea Hussein Kashoggi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Carthage na kumshusha Meoki, Fathi Meoki, mchumba wake, huko Medina, madukani. Meoki, 40, alitaka kununua zulia na vitu vingine vya ndani kwa ajili ya nyumba yao mpya, halafu Radia angempitia baadaye – baada ya kumshusha kamishna. Walivyotoka El-Manzeh, Radia na Meoki (wote warefu) walijitupa ndani Quadrifoglio (Alfa Romeo) nyeupe na kuondoka mpaka Barabara ya Ufaransa, mwanzoni mwa Place de la Victoire na ‘Bab el Bahar’ (lango la Medina), mkabala na Ubalozi wa Uingereza, ambako Meoki alishuka na kuingia madukani. Radia kisha akaendesha gari lake mpaka Carthage, nje ya mji, ambako pia ndiko alikoishi (yeye na shangazi yake) kumpokea  kamishna saa 9:40 adhuhuri.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...