Monday, 21 November 2016

Maisha Yako ni Sawa na Mto

200. Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.

Unapofikia hatua ya kuwa na kila kitu katika maisha, unapokuwa umefanya kila kitu ulichotamani kufanya katika maisha, unakuwa na bahari nzima ndani ya tone ambalo ni wewe. Unaridhika. Wewe si tone tena ndani ya bahari, wewe ni bahari ndani ya tone. Kinachobaki baada ya hapo ni kusaidia jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo, kuacha alama katika dunia kabla na baada ya wewe kuondoka, bila kujali watu watasema nini juu ya maisha yako.

Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.

http://www.facebook.com/koloniasantita

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...