Wednesday, 26 October 2016

Mojawapo ya Misingi ya Ujasusi

Mojawapo ya misingi ya ujasusi ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya unachojua, usichojua na unachofikiria. Unaweza kusema unajua wakati hujui. Maamuzi yasiyo sahihi ya kijasusi huweza kuiletea nchi madhara makubwa.

Watu wa usalama wanapaswa kuwa makini mno kwa sababu kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.

1 comment:

  1. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Tume ya Dunia Christoffer Sortevik, katika Ofisi ya Rais wa Tume ya Dunia jijini Copenhagen, baada ya Operation Devil Cross kuundwa, kwa ajili ya kumtafuta Panthera Tigrisi na wenzake wawili – Eduardo Chapa de Christopher na Gortari Manuel – mabilionea wa Hemisifia ya Magharibi.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...