Friday, 21 October 2016

Badilisha Maisha Yako

Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.

https://enockmaregesi.wordpress.com/badilisha/

3 comments:

  1. Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha. HBD Badilisha!

    ReplyDelete
  2. Mtu kufikia takdiri (/destiny/) yake lazima abadilishe maisha yake! Lazima! Bila hivyo, maisha yake yatambadilisha; kuwa mtu ambaye Shetani anataka awe, na si yule ambaye Mungu anataka awe.

    ReplyDelete
  3. Usipobadilisha maisha yako kuelekea kwenye takdiri yako utaishi kama Shetani anavyotaka, si kama Mungu anavyotaka.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...