Siku moja huko nchini Marekani mama mmoja aliamshwa usiku wa manane na jinamizi au ndoto ya kutisha. Shandalia iliyoning’inia chumbani kwa mtoto wake mchanga karibu na mlango ilianguka juu ya susu, kitanda cha mtoto, na kumuua! Saa ya redio pembeni mwa kitanda, akiwa bado yuko ndotoni, ilionyesha saa 10:35 za alfajiri. Kwa woga usio na kifani, yule mama, alipoamka, alimwamsha mumewe na kumwambia alichoota. Mumewe kwa bahati mbaya hakuwa muumini wa ndoto za kutisha, lakini alitaka kumwondolea shaka mkewe. Kwa hiyo alimwomba asiwe na hofu na alale, kwa sababu mtoto wao alikuwa salama.
Lakini yule mama hakupata tena usingizi. Hivyo alisimama kisha akaenda chumbani kwa mtoto wao na kumchukua mtoto, kisha akarudi naye mkapa kitandani kwao na kumlaza pembeni yake, halafu ndipo akalala tena.
Baadaye usiku, wazazi wote wawili waliamshwa tena. Lakini safari hii wakaamshwa na sauti kali ya dhoruba. Walisikia sauti kali ikitokea katika chumba cha jirani, hivyo wote wakakurupuka na kukimbia mpaka chumbani kwa mtoto wao. Shandalia iliyokuwa ikining’inia juu ya kitanda cha mtoto kumbe ilikatika na kuanguka juu ya susu, ambapo kwa bahati nzuri mtoto hakuwepo. Yule mama alivyoangalia saa, ilionyesha saa 10:35 za alfajiri.
Mfano huu wa jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kumsaidia mtu na kumwepusha na ajali au matatizo yoyote ni mzuri sana, asante kwa maisha yaliyookolewa. Kama angeidharau hii ndoto, yule mama angejuta maisha yake yote.
Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. ‘Madirisha’ madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya ‘maono’, au ‘mwako wa mwanga’ (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.
Ukiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemon’ (tofauti na ‘demon’) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria. 
Akili yangu itakaponipeleka kwa mgonjwa Muhimbili halafu sekunde hiyohiyo jicho langu likacheza au kiungo changu chochote cha mwili kikauma na kuacha ghafla ‘bila’ sababu yoyote, najua kile ninachokifikiria kuhusu mgonjwa huyo ama kitatokea au hakitatokea. Nikifikiria amepona, halafu ghafla kichwa kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake. Yaani, hatapona. Nikifikiria amekufa, halafu ghafla kichwa au kiungo kingine chochote kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake pia. Yaani, hatakufa. Hivyo, nikifikiria amepona, nikifikiria amekufa,  na kichwa kikaniuma na kuacha, sekunde hiyohiyo natakiwa kumwombea mgonjwa huyo. Kama ni kupona, apone kama Mungu alivyokusudia; na kama ni kufa, afe kama Mungu alivyokusudia. Si kama Shetani alivyokusudia. 
Kiungo chochote kikikuuma ghafla na kuacha au kikiendelea kukuuma kwa muda fulani halafu kikaacha, halafu huna sababu ya kwa nini kinakuuma, angalia unawaza nini wakati kiungo hicho kinakuuma. Kisha lifanyie kazi wazo hilo kwa maombi hata ya sekunde tano! Funika tatizo hilo, hata kama hulijui, kwa damu ya Yesu! 
Siku moja niliota ndoto. Nilikuwa Sinza Kumekucha (ndani ya ndoto) nikitembea kuelekea maeneo ya Shekilango. Lakini ghafla nikaona kioski cha soda pembeni mwa barabara, na muda huohuo nikapata hamu ya kwenda kununua kitu. Wakati nakunywa soda alikuja kaka mmoja mweupe amevalia kitanashati. Alivaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Hata hatukusalimiana. Lakini alinunua soda na keki akawa anakunywa huku akiangalia magari barabarani, na hakuwa na wasiwasi kabisa. Dakika chache baadaye alipita dada mmoja mzuri jirani na kioski kile akitembea kuelekea maeneo ya Sinza Palestina. Yule kaka alivyomwona, alishtuka. Alionyesha dhahiri kwamba alimtamani. Harakaharaka alimkimbilia yule dada na kuanza kuongea naye huku wakitembea taratibu kuelekea maeneo ya Hospitali ya Palestina. 
Nukta chache baadaye yule kaka na yule dada walivuka barabara na kwenda upande wa pili, ambapo daladala lilisimama kuwangojea. Kuona hivyo, nikaamua kuwafuatilia ili nijue mwisho wa safari yao. Nilikimbia na kupanda daladala walilopanda, bila hata kujua lilikokuwa likielekea. Daladala lilikuwa likielekea Kariakoo (najua daladala zinazopitia Sinza kutokea mjini huwa haziendi Kariakoo moja kwa moja lakini hii ilikuwa ni katika ndoto). Kufika Kinondoni, kwa Manyanya, baada tu ya ile barabara kubwa inayoelekea makaburini, yule kaka na yule dada walishuka na kuanza kutembea kuelekea katika nyumba moja iliyokuwa mkabala na kituo cha daladala. 
Lengo langu lilikuwa ni kujua kwa nini yule kaka alimchukua yule dada kirahisi vile na walikuwa wakienda wapi. Hali kadhalika nilishuka na kuendelea kuwafuatilia, lakini kwa kificho. Walipoingia katika nyumba ile iliyokuwa mkabala na kituo cha daladala nilibana sehemu. Lakini baadaye nami nikaingia katika nyumba hiyo, kupitia geti dogo, na kukuta ndani kuna basi kubwa bovu limeegeshwa karibu na ukuta. 
Nikiwa nimejificha, yule kaka na yule dada waliingia ndani ya lile basi lakini baadaye akatoka yule kaka peke yake bila ya yule dada. Hilo jambo lilinishangaza. Yule kaka alivyoingia ndani, ndani ya nyumba yake kubadilisha nguo, nilinyata hadi kwenye lile basi na kuingia ndani; ili nijue yule dada alikuwa akifanya nini mle. Lakini sikuona mtu. Nikajiuliza kuwa alikwenda wapi. Lakini kabla sijatoka ili niendelee na safari zangu nilisikia purukushani. Kuangalia vizuri, chini ya viti vya basi kulikuwa kumejaa watu akiwemo yule dada. Akili ikanambia hawa ni misukule. Yule kaka alivyorudi, nilishtuka kutoka usingizini. 
Tatizo langu sikufanya chochote kuhusiana na ile ndoto takatifu, takatifu kwa sababu niliiota kati ya saa tisa na saa kumi alfajiri. Lakini baadaye roho ilinisuta. Nilimpigia simu mchungaji mmoja wa kanisa la TAG la Upanga (Mchungaji Tina) ambaye ana kipawa cha kutafsiri ndoto. Tina alinitafsiria ndoto yangu yote. Kwa ufupi lile tukio lilitokea kweli katika ulimwengu wa roho, na kwa sababu sikumfunika yule dada kwa damu ya Yesu, lilitokea pia katika ulimwengu wa mwili. 
Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani utakapoamka mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua.

Msemo wa ‘Majuto ni mjukuu’ hauna maana yoyote kama utamsikiliza na kumfuata Roho Mtakatifu. Ukiwa na Roho Mtakatifu hakuna kujuta.
ReplyDeleteDo not ignore the calling of your heart.
ReplyDeleteUkiwa makini, nadhani, utapata maana ya ujumbe unaopewa na Roho Mtakatifu kwa wale wanaomwamini Mungu au ‘daemon’ (tofauti na ‘demon’) kwa wale wasiomwamini Mungu. Mimi, kwa mfano, huwa najali muda. Jicho langu likicheza au kiungo changu chochote cha mwili kikiuma ghafla na kuacha, au hata kisipoacha, jambo lolote ninalolifikiria muda huo ambapo jicho linacheza au kiungo changu cha mwili kinauma najua ni ujumbe kutoka kwa Mungu na una uhusiano na jambo hilo ninaloliwaza. Hivyo, kuanzia sekunde hiyo napaswa kuwa makini sana na jambo lolote ninalolifikiria.
ReplyDeleteAkili yangu itakaponipeleka kwa mgonjwa Muhimbili halafu sekunde hiyohiyo jicho langu likacheza au kiungo changu chochote cha mwili kikauma na kuacha ghafla ‘bila’ sababu yoyote, najua kile ninachokifikiria kuhusu mgonjwa huyo ama kitatokea au hakitatokea. Nikifikiria amepona, halafu ghafla kichwa kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake. Yaani, hatapona. Nikifikiria amekufa, halafu ghafla kichwa au kiungo kingine chochote kikaniuma na kuacha, kitakuwa kinyume chake pia. Yaani, hatakufa. Hivyo, nikifikiria amepona, nikifikiria amekufa, na kichwa kikaniuma na kuacha, sekunde hiyohiyo natakiwa kumwombea mgonjwa huyo. Kama ni kupona, apone kama Mungu alivyokusudia; na kama ni kufa, afe kama Mungu alivyokusudia. Si kama Shetani alivyokusudia.
Kiungo chochote kikikuuma ghafla na kuacha au kikiendelea kukuuma kwa muda fulani halafu kikaacha, halafu huna sababu ya kwa nini kinakuuma, angalia unawaza nini wakati kiungo hicho kinakuuma. Kisha lifanyie kazi wazo hilo kwa maombi hata ya sekunde tano! Funika tatizo hilo, hata kama hulijui, kwa damu ya Yesu!
Siku moja niliota ndoto. Nilikuwa Sinza Kumekucha (ndani ya ndoto) nikitembea kuelekea maeneo ya Shekilango. Lakini ghafla nikaona kioski cha soda pembeni mwa barabara, na muda huohuo nikapata hamu ya kwenda kununua kitu. Wakati nakunywa soda alikuja kaka mmoja mweupe amevalia kitanashati. Alivaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Hata hatukusalimiana. Lakini alinunua soda na keki akawa anakunywa huku akiangalia magari barabarani, na hakuwa na wasiwasi kabisa. Dakika chache baadaye alipita dada mmoja mzuri jirani na kioski kile akitembea kuelekea maeneo ya Sinza Palestina. Yule kaka alivyomwona, alishtuka. Alionyesha dhahiri kwamba alimtamani. Harakaharaka alimkimbilia yule dada na kuanza kuongea naye huku wakitembea taratibu kuelekea maeneo ya Hospitali ya Palestina.
ReplyDeleteNukta chache baadaye yule kaka na yule dada walivuka barabara na kwenda upande wa pili, ambapo daladala lilisimama kuwangojea. Kuona hivyo, nikaamua kuwafuatilia ili nijue mwisho wa safari yao. Nilikimbia na kupanda daladala walilopanda, bila hata kujua lilikokuwa likielekea. Daladala lilikuwa likielekea Kariakoo (najua daladala zinazopitia Sinza kutokea mjini huwa haziendi Kariakoo moja kwa moja lakini hii ilikuwa ni katika ndoto). Kufika Kinondoni, kwa Manyanya, baada tu ya ile barabara kubwa inayoelekea makaburini, yule kaka na yule dada walishuka na kuanza kutembea kuelekea katika nyumba moja iliyokuwa mkabala na kituo cha daladala.