Wednesday, 19 October 2016

Taifa Halitasimama Kupigana na Taifa

Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita hutengenezwa ndani ya mioyo ya watu. Ukiitafuta amani ndani ya moyo wako, taifa halitasimama kupigana na taifa, amani itaweza kupatikana.

Kama George Bush angekuwa na amani ndani ya moyo wake na Saddam Hussein angekuwa na amani ndani ya moyo wake Vita ya Ghuba isingetokea. Vilevile, katika kitabu cha Kolonia Santita, kama Rais wa Tume ya Dunia angekuwa na amani ndani ya moyo wake na kiongozi wa Kolonia Santita angekuwa na amani ndani ya moyo wake Kolonia Santita isingepigana na Umoja wa Mataifa. Taifa lisingepigana na taifa, na mataifa yasingepigana na magaidi.

2 comments:

  1. Taifa halitasimama kupigana na taifa kama watu wote watakuwa na amani ya nafsi.

    ReplyDelete
  2. Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie! Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Adui Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa! Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...