196. Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu
anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama
wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu
kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya
damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.
Kusudi mimba itungwe lazima kuwepo na kromosomu X na kromosomu Y.
Kromosomu ni nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni au DNA, ambazo
hubeba taarifa kuhusu sifa za kimaumbile zinazorithishwa kwa kiumbe hai
kutoka kwa mama na baba wa kiumbe hicho. Kwa upande wa Yesu Kristo,
katika hali ya kawaida, kromosomu X ilitoka kwa Maria Magdalena na
kromosomu Y ilitoka kwa malaika Gabrieli. Yesu alikuwa Myahudi lakini
Kristo ni Mungu. Yesu Kristo alikuwa binadamu kama sisi, lakini alikuwa
na utukufu na alikuwa na damu ya Mungu iliyotakasika. Damu kama hiyo
ndiyo inayotiririka katika miili ya kila mmojawetu ijapokuwa ni damu ya
Adamu, ambayo bado haijatakaswa. Damu ya Yesu si kitu kidogo.
Ilipomwagika msalabani ilifunika dunia nzima. Ndiyo maana tukasamehewa.
Bila damu hiyo, bila utukufu huo wa Mungu, hakuna binadamu
atakayeokolewa, hakuna pepo atakayeondolewa.
Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi
wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua
mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa
adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu
ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa
damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza
kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani
atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa
ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya
aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo
Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.
Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa
binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi makanisani na misikitini.
Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza dhambini huku tunaona, tukiwa
mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu.
Mungu anaishi ndani ya damu, maisha ya Mungu yalikuwa yanaishi ndani
ya mwili wa Yesu Kristo, anaishi ndani ya miili yetu. Unapokula damu,
unapokunywa damu, unakula, unakunywa sehemu ya Mungu aliyekuumba.
Kama damu haina maana kwa nini Mungu anaipenda? Kama damu haina maana
kwa nini Shetani anaipenda? Mungu ni roho, Shetani ni roho, lakini damu
ni kitu kinachoonekana kwa macho. Kwa nini damu ni kitu cha muhimu
kiasi hicho kwa Mungu na kwa Shetani pia? Damu ni pato la ziada la
ufunuo wa kiroho. Yaani, damu ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mungu
ndiye aliyetengeneza damu kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe, hata
Shetani hajui kwa asilimia mia umuhimu wa damu katika ulimwengu
unaoonekana na katika ulimwengu usioonekana. Damu ina uwezo wa kuzuia
mapepo kutoka kuzimu yasiharibu mipango ya maisha ya watu na ina uwezo
wa kuondoa dhambi. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi. Jibu la tatizo
hilo ni damu ya Yesu Kristo.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...

Shetani anapenda damu kumdhihaki Mungu kwa sababu Mungu anapenda damu na bila damu hakuna binadamu atakayeokolewa. (Bila damu wokovu hauna maana). Usimwogope Shetani eti kwa sababu anapenda damu, mwogope Mungu kwa sababu ndiye anayejua umuhimu wa damu hiyo.
ReplyDelete