Kuna mafanikio ya aina mbili hapa duniani: Mafanikio ya Shetani na
mafanikio ya Mungu. Mafanikio ya Shetani ni rahisi kupata na ni ya
kitumwa. Mafanikio ya Mungu ni magumu kupata lakini ni ya hakika. Mungu
akikubariki, pesa inaongezeka kama inavyoongezeka saa.
Ukiwa
na mafanikio ya Shetani hayo si mafanikio ya kweli. Ukiwa na mafanikio
ya Mungu hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Mafanikio ya kweli hayatokani
na NINI unacho. Mafanikio ya kweli yanatokana na NANI unaye. Yesu
Kristo alikuwa maskini, hakuwa na kitu; lakini alikuwa tajiri, alikuwa
na Mungu ndani ya moyo wake.
Yusufu alikuwa hohehahe kabla na
baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa,
hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile
alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu
alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na
Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo
utakaotutafuta sisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...

Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.
ReplyDelete