Friday, 18 December 2015

EAEP

Kutoka kushoto: Dkt Lizzy Attree, Enock Maregesi, Ruth Wangari (mhariri wa Kiswahili wa Kampuni ya Uchapishaji wa Vitabu ya EAEP ya Kenya), Profesa Abdilatif Abdalla (mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Uandishi wa Vitabu ya Jomo Kenyatta 1974), Anna Samwel Manyanza, Profesa Mukoma wa Ngugi. Kampuni ya Uchapishaji wa Vitabu ya East African Educational Publishers Limited (EAEP) itachapisha miswada ya KOLONIA SANTITA na PENZI LA DAMU kama vitabu ifikapo mwezi wa Agosti 2016 – kabla ya kutangazwa kwa washindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika 2016 popote tutakapotangaziwa. EAEP watachapisha vitabu hivyo katika ubora wa kimataifa.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com 

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...