Thursday, 17 December 2015

Mukoma wa Ngugi

Mimi, Profesa Ken Walibora na Profesa Mukoma wa Ngugi (mtoto wa Profesa Ngugi wa Thiong’o wa Kenya) baada ya mimi na Mukoma kuhojiwa na Ken kuhusiana na Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika, katika Hoteli ya Serena Nairobi. Mukoma wa Ngugi ni profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Cornell cha New York nchini Marekani. Yeye na Dkt Lizzy Attree (mkurugenzi wa tuzo ya juu zaidi kati ya tuzo zote za uandishi wa vitabu barani Afrika ya Caine) ndiyo waanzilishi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika iliyoanzishwa huko Nijeria mwaka 2014.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...