Bomu la mkono lililotumiwa na Kamanda wa Operation Devil Cross Meja John Murphy Ambilikile wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Gruneti, lililotumika kubomolea lango kuu la jumba la utawala la Kolonia Santita katika Msitu wa Benson Bennett nchini Meksiko, kabla ya Vijana wa Tume kuingia katika vyumba vinne vya usalama vya jumba la utawala – walipotakiwa kupigana kwa mikono mitupu na maadui zaidi ya mia moja – kabla ya kufika katika ofisi ya Panthera Tigrisi ya Salina Cruz, Oaxaca, ambapo hata hivyo walikuta HVT ametoroka kuelekea Gwatemala.
http://www.enockmaregesi.wordpress.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...

Ndani ya gruneti kuna vitu kumi vyenye uwezo na visivyokuwa na uwezo wa kulipuka kama vile pini, mtaimbo, springi ya mtaimbo, tundu la kuingizia baruti, baruti, fataki, fyuzi, utambi, wenzo na ganda la chuma la pingili kama vipande vya risasi. Pini inapochomolewa, na bomu kurushwa kuelekea kwenye shabaha au kuelekea sehemu nyingine yoyote, wenzo wa usalama huchomoka pia na kuachana na bomu moja kwa moja. Wenzo wa usalama unapochomoka huruhusu mtaimbo ugonge fataki ya kuwashia fyuzi kwa nguvu na kasi kubwa. Fyuzi itawaka kwa sekunde nne kabla ya kuwasha utambi, ambao utawasha baruti ndani ya sekunde moja, kabla ya baruti kulipuka – na kusambaza vipande vya bomu katika kila sehemu ya shabaha.
ReplyDelete