Monday, 10 August 2015

Moyo

149. Maskini hajali wewe ni nani. Anajali utu ndani ya moyo wako.

http://www.facebook.com/koloniasantita

1 comment:

  1. Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako.

    Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.

    Mungu alimpa kila mmoja wetu vipawa na vipaji vya pekee kwa ajili ya huduma yake. Kazi yake kwetu hapa duniani ni kutumia vipawa na vipaji vyetu kwa ajili ya huduma ya watu wengine. Kila mmoja wetu ana kitu fulani anachoweza kutoa kwa ajili ya mtu mwingine mwenye shida. Tunaweza kutoa pesa zetu na muda wetu kwa watu maskini. Tunaweza kuwa marafiki kwa watu wapweke au watu wasiojiweza kiafya. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya mabadiliko ya watu wengine. Tunaweza kuwa wasuluhishi wa migogoro ya amani. Tunaweza kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote kwa familia zetu. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea au kazi za kuajiriwa kwa uadilifu, uaminifu, heshima, na upendo kwa wengine.

    Kila binadamu hapa duniani ni wa thamani kubwa. Chochote utakachofanya, kizuri au kibaya, kidogo au kikubwa, kitabadilisha maisha ya watu. Ukitoa kidogo kwa moyo mmoja inatosha. Ukitoa kingi kwa moyo mmoja inatosha pia. Kuwa mkarimu kwa mazingira, kuwa mkarimu kwa wanyama, kuwa mkarimu kwa binadamu wenzako, kwa faida ya vizazi vijavyo.

    Ukienda katika kituo cha watoto yatima halafu watoto wakakulilia shida zao na ukaondoka bila kuwasaidia chochote, hutalala vizuri usiku.

    Kujitolea kwa moyo mmoja kwa muda mrefu huleta furaha na afya njema kwa mtoaji na kwa mpokeaji pia.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...