Thursday, 13 August 2015

Metropol

Hoteli kubwa iliyopo katikati ya Moscow karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo kabisa ya Kitay-gorod, kitovu cha biashara cha Moscow ya kale, na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy na Ikulu ya Moscow ya Kremlin, Hoteli ya Metropol, John Murphy aliposhuka baada ya teksi yake kuharibika akielekea katika ofisi za Tume ya Dunia za Smolenskaya Prospekt za jijini Moscow – akitokea katika Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo – ambapo alitekwa nyara na Kolonia Santita na kupelekwa Yugo Zapadnaya kunyanyaswa, lakini akaokoka kwa kutumia Stinger, katika mazingira ya kutatanisha.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com

1 comment:

  1. John Murphy alifika Moscow tarehe 1/11/1992 saa 11 alfajiri akitokea Cairo, Misri. Wakati huo Moscow kulikuwa na baridi sana. Teksi yake ilipofika Teatralny Proezd, upande wa kusini wa Hoteli ya Metropol – karibu na mojawapo ya minara ya mwanzo ya Kitay-gorod, kitovu kikuu cha biashara cha Moscow ya kale – kwa matatizo ya injini; magaidi wanne, waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya Bentley Continental S nyeusi – iliyokuwa na namba za kitemi za B 001 BB 77 RUS mali ya Kiongozi wa CS-Moscow Dmitri Olegushka – toka Uwanja wa Ndege wa Sheremetyevo II wa kaskazini-magharibi mwa jiji la Moscow, waliendelea mbele na kusimama mkabala na Jumba la Maonyesho ya Tamthilia la Bolshoy; kisha wawili kati yao wakashuka na kuingia ndani ya kioski, wawili wakibaki ndani ya gari kuhakikisha John Murphy hawapotei. Magaidi hao wa CS-Moscow, Tawi la Kolonia Santita la Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini, walijua Murphy alishawahisi.

    Murphy hakupenda kusubiri eti mpaka gari itengamae. Alikuwa akichelewa na alikokuwa akienda hakukuwa mbali kutokea hapo. Hivyo alishuka baada ya kulipa nauli, na kutembea kuelekea Smolenskaya; karibu na mtaa maarufu ulimwenguni wa wenda kwa miguu wa Arbat, na makasri ya Ikulu ya Shirikisho la Urusi, katika ofisi za Tume ya Dunia.

    Kama kuna swali maarufu kuliko yote katika kitabu cha 'Kolonia Santita' ni "Кто Вы, где Вы от, и почему Вы в Москве?" lililoulizwa na товарищи (Komredi) Anatoly-Chaika, baada ya kumfikisha Murphy katika 'dacha' ya Kolonia Santita ya Yugo Zapadnaya. Murphy hakumwelewa Chaika. Lakini mwenzake na Chaika (Vladimir) alipouliza kwa tafsiri, "Wewe ni nani, unatoka wapi, na unafanya nini Moscow?" Murphy alimwelewa na kucheka akiwa amenuna. Bila swali hilo asingeokoka.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...