Monday, 3 August 2015

Kipaji

148. Ningependa – maisha yangu yatakapokoma hapa duniani – kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. Nilijifunza toka awali umuhimu wa kushindwa katika maisha ijapokuwa nilijitahidi sana, na nilipoendelea kushindwa niliweka nadhiri ya kufanya kitu kimoja kilicholeta maana zaidi katika maisha yangu nacho ni uandishi wa vitabu. Uandishi wa vitabu ndicho kitu pekee nilichokiweza zaidi kuliko vingine vyote na kuanzia hapo Mungu aliniweka huru. Nilijua mimi ni nani. Nilijua kwa nini nilizaliwa. Nilijifunza falsafa ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko nilivyoikuta – kwa sababu hata mimi nilikuwepo – na falsafa ya kushindwa si hiari. Maarifa hayo yakafanya niwe na heshima na upendo kwa watu wote.

    Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu.

    Mungu anapokupa kipaji anategemea ukitumie vizuri kwa ajili ya wengine. Usipokitumia vizuri kwa ajili ya wengine, ama kwa uvivu au kwa woga, atawapa wengine wakitumia kwa ajili yako. Ukitumia vipaji vyako vizuri, Mungu atakuongezea maradufu. Yaani, ukitumia muda wako vizuri atakuongezea muda. Ukitumia nguvu zako vizuri atakuongea nguvu. Ukitumia pesa yako vizuri atakuongezea pesa. Ukitumia ukarimu wako vizuri atakuongezea ukarimu. Ukitumia maarifa yako vizuri atakuongezea maarifa.

    Watu waliyofanikiwa zaidi katika maisha ni wale waliyotumia vipaji vyao vizuri, walivyopewa na Mungu.

    ReplyDelete
  2. Ukitaka kujua vipaji vyako ulivyopewa na Mungu mtumikie Mungu katika kitu fulani kwa nguvu zako zote.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...